Taswira Za Waziri Wa Habari, Utamaduni Na Michezo Akiwa Na Wajumbe Wa Kamati Ya Utendaji Wa Mabaraza Ya Habari Duniani.


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara akiongea na kubadilishana business cards na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Muungano wa Mabaraza ya Habari Duniani waliomtembelea ofisini kwake leo  Jijini Dar es Salaam. Wajumbe hao kutoka nchi kumi na moja (11) Duniani wako hapa nchini kwa ajili ya mkutano wa mwaka  ambao utafanyika kesho kutwa  katika Mbuga ya wanyama  ya Mikumi.Wenyeji wa mkutano huo ni Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara akitazama zawadi aliyokabidhiwa na Mjumbe wa Chama cha Waandishi wa Habari kutoka Uturuki, Bw. Ali Hancerli.  Bw. Hancerli ni mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Muungano wa Mabaraza ya Habari Duniani waliomtembelea Mhe. Waziri leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Wajumbe hao, wapo hapa nchini kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka chini ya uenyeji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (aliyevaa koti jeusi) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Muungano wa Mabaraza ya Habari Duniani walipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Pembeni ya Mhe. Waziri kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga. Wajumbe hao kutoka nchi kumi na moja (11) Duniani wako hapa nchini kwa ajili ya mkutano wa mwaka ambao utafanyika kesho kutwa katika Mbuga ya wanyama ya Mikumi.Wenyeji wa mkutano huo ni Baraza la Habari Tanzania (MCT).


         Picha na Concilia Niyibitanga - Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.