JINAMIZI linazidi kuwaandama wasanii wa tasnia ya filamu baada ya mwanadada mwenye mikasa kutoka Bongo movie Wema Sepetu kumwaga chozi back stage wakati mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo fleva Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ alipopanda Jukwaani na kusema Bongo fleva ni kicheche kama Wema Sepetu.
Wema Sepetu akiwa na Steven Nyerere jukwaani katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Wasanii wa Bongo movie wakisakata muziki katika uwanja wa CCM Kirumba
Chanzo chetu cha habari kimesema
kuwa Ney alipopanda Jukwaani na kuchana freestyre na kulinganisha
Bongofleva kicheche kama Wema Sepetu umati uliokuwa uwanjani ulilipuka
kwa furaha na kumshangilia Ney akiwa sambamba na Dallaz Ukuni
mwanamuziki mwenzake.
Kufuatia hali hiyo Jacob Stephen ‘JB’,
Aunt Ezekiel wakiwa na Steven Nyerere walizua zogo lilotengeneza fujo
wakitaka kumvamia Ney na kumpiga huku JB akilalama kwa kusema kuwa Ney
amekuwa akiwadhalilisha kwa kutumia nyimbo zake.
Wakati hayo yakifanyika Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’ alionyesha busara zake kwa kutoshiriki ugomvi huo.
.
Msanii wa muziki wa Bongofleva aliyemliza Wema Sepetu kwa kuufananisha muziki wa Bongo fleva kicheche kama Wema Sepetu.
Aunty Ezekiel akisakata Rumba na Wema Sepetu.
Aunty Ezekiel na Wema wakiwa wamejiachia
“Sasa hawa
mbona wanataka kutuharibia show yetu vipi? Kwanza huyu aliyeitwa
kicheche hata hajamaindi lakini wapambe ndio nawaona wanataka
kulianzisha mbona mwenzao Ray katulia?" alihoji Samson Masanja mkazi wa Mwanza.
Pamoja na sakata hilo show ilibamba kwa
msanii Ney wa Mitego Dallaz Ukuni kufanya bonge la show sambamba na
wasanii wengine wakali wa Bongo fleva kama Roma, Fid Q, Bob Junior,
Mwasiti, Godzilla, Barnaba, Pro. Jay, Recho, At na Nyota kutoka THT.