WASANII WAENDELEA KUNUFAIKA NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NA HIVI SASA NI ZAMU YA LINEX NA KEKO WA UGANDA


Inaonekana kama Jumuiya ya Afrika Mashariki inaendelea kutumiwa vyema na wasanii wa nchi wanachama katika kupeana support kwenye nyimbo zao. 

Linex anayeiwakilisha 255 ameamua kumtafuta rapper wa kike wa Uganda Keko kwa collabo moja ya hatari sana. Hatupati picha mchanganyiko wa code hizi 255 + 256 = ? Definetely a monster HIT!

Jumapili,Mpekuzi imepata nafasi ya kuisikiliza ngoma hiyo (exclusively) ukifanyiwa mixing kwenye studio za Classic Sounds na producer Mona G and we can assure you that, it’s gonna be a mojor hit.

Linex ameonesha uwezo mkubwa sana kwenye ngoma hiyo yenye mahadhi ya R&B kitu ambacho ni sababu tosha ya kwanini ameamua kufanya collabo na Keko.


Wimbo huo hivi karibuni utatumwa jijini Kampala, Uganda ili Keko aingize kipande chake na hatimaye urudi tena Bongo kwaajili ya mixing ya mwisho na uwe tayari kuhit the waves!