
Ndugu zangu, 
Kuna
 wenzetu kadhaa walioniandikia kutaka niandae utaratibu wa kukusanya 
michango ili imfikie mjane wa Marehemu Daud Mwangosi ambaye sasa 
anakabiliwa na jukumu kubwa la kuwalea watoto wanne baada ya kuondokewa 
na mumewe.
Ninachopendekeza;
Kwa
 vile ni ukweli ambao hata mimi nilipokuwa msibani jana niliusikia; 
changamoto ya mjane wa marehemu kutunza watoto. Nadhani njia nzuri ya 
kumsaidi mjane huyu wa marehemu ni kwenye suala la elimu ya watoto wake 
wanne ambaye wa mwisho ana miama miwili tu.
Yakufanya:
1. Tusubiri kwanza mjane arudi Iringa kutoka kumzika mumewe huko Tukuyu.
2.
 Mimi nitakwenda kwa mjane na kumwelezea dhamira ya baadhi yenu  humu 
kijijini Mjengwablog kutaka kumsaidia japo kwa kuchangia elimu ya watoto
 wake.
3. Aniambie ni watoto wake wangapi walio shuleni na kiasi gani kinahitajika kwa ada ya muhula au mwaka.
4.
 Wenye kujisikia kumchangia wafanye hivyo kwa kupitia akaunti yake 
ikiwamo M- Pesa, Tigo Pesa  na Airtel Money kama anazo zote. Vile vile 
kwa Western Union.
5.
 Michango hiyo itumwe moja kwa moja kwake na yeye atunze kumbukumbu ya 
waliomchangia na  anijulishe pale kiasi kinachohitajika kama 
kimepatikana au la. Nami nitawajulisha juu ya hilo kupitia hapa.
Ni hayo tu, nakaribisha michango yenu ya maoni.
Mwenyekiti Wenu, 
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
 
