WILSHERE KUREJEA UWANJANI KARIBUNI.
KIUNGO wa klabu ya
Arsenal, Jack Wilshere anatarajiwa kuongeza nguvu katika kikosi cha
Arsenal Wenger wakati atakapoanza rasmi mazoezi na klabu hiyo wiki hii. Wilshere
mwenye umri wa miaka 20 amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya kifundo cha
mguu ambayo yamesababisha kuwa nje ya uwanja toka Agosti mwaka 2011
lakini kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza anatarajiwa kusahau yote
hayo na kurejea uwanjani tena. Nyota alikuwa tayari ameanza mazoezi
mepesi na kuonyesha maendeleo mazuri hivyo anatarajiwa kujiunga na
wachezaji wenzake wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mazoezi mwishoni mwa
wiki hii. Klabu imepanga kujaribu kumchezesha kiungo huyo katika baadhi
ya michezo ya kirafiki mazoezini au katika kikosi cha timu hiyo cha
vijana chini ya miaka 21 ambacho kitapambana na West Bromwich Octoba
mosi ili kujaribu kumrejesha katika kiwango chake cha awali.