
Si
ajabu ulishakutana na vijana mjini waliovaa nguo na suruali zinazobana
na ambazo zinakaribia kuanguka viunoni kwasababu ya mtepesho wa hatari
kama Lil Wayne! Ama ulishakutana na msichana wa miaka 16 akiwa
ametengeneza kope zake kwa kuzipaka rangi za ajabu ajabu ili afananane
na Nicki Minaj!
Kitu cha kawaida zaidi kukutana na vijana waliovaa t-shirt zilizoandikwa YMCMB (Young Money Cash Money Billionares).
Sio
kila mtu anafurahia mavazi ya wasanii hao wa Marekani. Infact, rapper
Nikki Mbishi aka Baba Malcom, anawalaumu wasanii wa YMCMB kwa kuharibu
vijana wa Tanzania.
“Hawa wadwanzi YMCMB ndo wamesababisha watoto wa kiume kuvaa mavazi ya kike na visuruali kama condoms,mbaya
zaidi rangi zao ni njano,kijani,nyekundu,pink,purple,orange mpaka aibu
mitaani,ukija kwenye hair cutz ndo mama yangu,mara rangi ya njano,pink
n.k yaani ni MASHOGA TASLIMU!!!,” alisema Nikki kupitia Facebook.