Lad Jaydee
Majina ya Diamond na Lady Jaydee yanaweza kuwa miongoni mwa majina ya
wasanii wa Tanzania yaliyoonekana kwenye mitandao mingi zaidi ya nje. Umaarufu wa wasanii hawa hauwezi kuepukika na Diamond akiongoza msafara.Mtandao maarufu wa MSN ambao ndio dada wa anuani maarufu duniani ya hotmail jana imeandika habari picha iliyopewa jina la ‘The King and Queen of Bongo Flava’ na kuwataja Diamond na Lady Jaydee kama vinara nchini Tanzania.
“Bongo Flava is a genre of hip hop from Tanzania. The lyrics are in English or Swahili. Two of the biggest stars of this genre are Diamond Platnumz and Lady Jaydee,”umeandika mtandao huo kwenye page maalum kuhusu mambo ya Afrika ya ‘http://african.howzit.msn.com’ ambayo ni sehemu ya MSN inayoandaliwa nchini Afrika Kusini.