Ndugu zangu wanamichezo wa nchi hii, ni
ukweli usiofichika hii filamu ya mashabiki wa simba juu ya tuhuma za
kipa wao aliyetumikia timu yao kwa kipindi kirefu na kuwapa mafanikio
mengi ikiwemo ubingwa ligi kuu ni filamu mbovu kuwahi kutokea katika
nchi hii,
Filamu hii niliyoibatiza jina Kaseja
& Simba Fans ni filamu ambayo haina mvuto haileweki washiriki
inaonekana hawakujiandaa vyema kushiriki filamu hii inaonyesha wazi
washiriki wasivyo na talent kama ilivyokuwa kwa kina marehemu steven
kanumba, vicent kigosi, Monalisa na wengine wengi wa kwenye tasnia ya
Bongo Movie.
Filamu hii imebeba ujumbe wa ya kuwa
kaseja sasa hatakiwi kuitumia timu ya simba, haina utofauti na filamu
fulani ya nchini Nigeria mtoto ambaye alikataliwa kwao ila wale
wanaigeria waliweza kufikisha ujumbe katika jamii kupitia filamu yao
ile, maana katika jamii wapo watu wanaofukuza watoto zao hata kwa kisa
ambacho kinavumilika leo usishangae mama kamchoma mwanae tena wa kumzaa
mikono kwasababu kadokoa nyama jikoni.
Tujiulize ndugu zangu watanzania
mashabiki wa soka je kupitia filamu hii ya kaseja & simba fans
tumepata ujumbe gani kama jamii ya wapenda michezo je hali hii
inafundisha nini kizazi cha kesho katika tasnia ya michezo ya nchi hii,
mimi nashauri mashabiki wa simba warudi kwa director wao wa Filamu hii
waandike upya script watoe part 2 itakayoonyesha kurudisha imani kwa
kipa wao namba moja Juma Kaseja ili mzunguko wa pili wa ligi hali isije
kuwa mbaya zaidi.
Pamoja tujenge michezo