"NINA UHURU WA KUTOA PENZI KWA MTU YEYOTE NINAYEMPENDA.....WANAODAI NATEMBEA NA WAUME ZA WATU NI WANAFIKI".......AGNESS MASOGANGE
MWANADADA anayejipatia umaarufu kupitia video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya,
Agness Masogange, ameuambia mtandao huu kuwa hatumii mwili wake kama chombo cha kuwakamata wanaume bali hutoa
penzi lake kwa yule anayempenda na ishu zinazozungumzwa mitaani kuwa
anaongoza kwa kuiba wanaume za watu si kweli na wanaodai
hivyo hawamtakii mema.Mwandishi wetu alizungumza na mwanadada huyo juu ya ishu kadhaa
zinazongumzwa juu yake, ndipo alipofunguka kuwa hatumia uzuri wake au
umbo lake kama njia ya kuwavuta wanaume kwani angeamua kufanya hivyo
basi angekuwa na wanaume wengi sana.
“Mwili wangu si chombo cha kuwakamata wanaume na hao watu wanaosema
kuwa naongoza kwa kutembea na wanaume za watu ni wale wenye nia ya
kunichafua kwani mi si demu wa hivyo,” alidai