"ALIYEKUWA AKISAMBAZA PICHA ZANGU ZA UCHI NI MPENZI WANGU"...RAYUU

MSANII aliyeshika kasi baada ya picha zake zilizokuwa zinamuonesha sehemu kubwa ya mwili wake kuvunja, Rayuu amesema kuwa baada ya kufanya uchunguzi juu ya ishu hiyo amegundua kuwa mtu aliyekuwa anasambaza picha zake ni mpenzi wake ambaye kwa muda mwingi walikuwa kwenye mzozo mkubwa uliosababisha kuachana kwao.Msanii huyo ameuambia mtandao huu kuwa uchunguzi huo ulifanywa na moja ya ndugu zake pamoja na rafiki zake wa karibu, ambapo walikuja kujua ni mpenzi wake huyo baada ya kuona moja ya ujumbe kwenye simu yake aliokuwa anamtumia mwandishi mmoja wa habari kuhusiana na picha hizo.

Msanii huyo alidai kuwa baada ya kuona hivyo hawakufanya lolote kwani walikuwa wanaendelea na uchunguzi na walikuja kuzikuta picha za Rayuu nyingi kwenye laptop yake kitu ambacho kilimfanya ashindwe kuelewa ni kwa nini alikuwa anamdhalilisha kiasi hicho.
Rayuu alisema alikuwa anahisi simu yake imeibiwa na mtu mwingine kumbe mpenzi wake huyo ndiye aliyekuwa amechukua na hata alipokuwa anamuliza kuhusiana na simu hiyo hakuna ushirikiano wowote aliokuwa anampa kitu ambacho kimesababisha hata mapenzi yao kuvunjika.

“Sikuamini kwa ishu ambayo imetokea kwa sababu mpenzi wangu hakuwa katika akili yangu kama anaweza kufanya kitu kama hicho, lakini kabla hapo tuliwahi kuwa na mzozo mkubwa nahisi alitumia nafasi hiyo ili kunionesha kwamba anaweza kunichafua,” alisema.

Msanii huyo ametoa ushauri kwa wanawake wengine kuwa wakiwa na wapenzi wao wasijaribu kupiga picha za aina hiyo kwani wapo wanaume wengine ambao huzitunza picha hizo kwa makusudi yake, kama alivyofanyiwa yeye.