KIZITO
Mahamba (50) (pichani), mkazi wa Mwananyamala Mtaa wa Msili B jijini
Dar es Salaam, amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala wodi namba 5A
baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha na mkewe ambaye amemmwagia maji ya
moto mwilini.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii huku akiwa katika hali mbaya wodini alikolazwa, Mahamba alidai kuwa mkewe, Rabina Mkakamba (38) kabla ya kufanya tukio hilo alianza kuonyesha dalili za kumdharau kila alipojerea nyumbani.
“Siku ya tukio ambayo ilikuwa Oktoba 20, mwaka huu, mke wangu hakuwa
katika hali ya kawaida maana kila nilichomwagiza kufanya alikataa,
nikajiuliza kulikuwa na nini?
“Hayo yote yalipokuwa yakiendelea, jikoni alikuwa anachemsha maji, nikiwa nimelala nilishitukia mke wangu akiingia chumbani na chupa ya chai ambayo alinitupia na maji kuniunguza sehemu kubwa ya mwili wangu, nadhani alitaka kuniunguza usoni.
Baada ya kufanya kitendo hicho alichukua sanduku la nguo zake na fedha zangu na kutoweka huku akiniacha nikigaagaa .
“Nililetwa hapa hospitali na mtoto wa ndugu yangu na ndiye anayenisaidia,” alisema Mahamba.