WAKATI watanzania wengi wakiamini kuwa msanii Ney Wa Mitego, yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanadada wa kwenye tasnia ya filamu Salma Jabu ’Nisha’, mkali huyo
amekanusha uwepo wake kwenye mahusiano na mwanamke yeyote na kudai kuwa
kwa sasa ana marafiki tu wa kike wa kubadilishana mawazo na si wapenzi
au mpenzi kama watu wanavyodai.Hata hivyo kauli ya msanii huyo inaweza kuzua utata mkubwa kwani
mashabiki wake wengi wanajua kuwa mpenzi wake ni mwanadada huyo wa bongo
movie ingawa tangu kutoka kwa habari hizo hakuwahi kuzungumza lolote
juu ya mahusiano hayo kama ni kweli.
“Hapana kwa sasa sina mpenzi, nimeshatoka na wanawake kadhaa hilo lipo wazi lakini kwa sasa natafuta yule mpenzi mwenye tabia njema,” alisema.
“Hapana kwa sasa sina mpenzi, nimeshatoka na wanawake kadhaa hilo lipo wazi lakini kwa sasa natafuta yule mpenzi mwenye tabia njema,” alisema.