Shumileta |
Wakati alipozungumzia juu ya wasanii wanaojiunza kwenye hoteli kubwa kubwa, mwandishi wa mtandao wa DarTalk alitaka kujua kiundani ishu hiyo, ndipo alipodai kuwa wapo baadhi ya nyota wanaofanya kazi hiyo kwa kuwa hawaithamini miili yao na ndiyo maana wanafanya hivyo.
Akiongea na DarTalk, Shumileta alidai kuwa uwepo wake kwenye game kwa muda mrefu kumemfanya ajifunze mambo mengi na huwa anashika kichwa pale anapowaona wasanii waliokuja juzi kwenye tasnia hiyo wakijiona kama wakongwe wakati hakuna kitu wanachokijua.
Alisema kuwa yapo mabaya mengi anayoyajua lakini wasanii wengine anapowaelekeza wamekuwa wajuaji sana hivyo anawaacha na anawachukulia kama wao wanavyotaka, lakini wengi wanapotea kutokana na kutojua wanatakiwa waishi vipi ili kwenda sawa na umaarufu walionao.
“Ukubwa dawa unajua kuna wasanii wamekuja jana lakini wanashindwa kuelewa kwamba yule uliyemkuta lazima umpe heshima yake wao hawajui hilo, kwa sababu tu wanafanya vizuri majina yanajulikana basi, lakini kuna mambo ambayo wanafanya wanapotea na watu kama sisi tunayajua lakini tunashindwa kuwaambia kwa sababu wanakauli za kuudhi,” alisema