Hivi
karibuni watu wanaosadikika kuwa ni wapinzani wa rais Obama wametoa
toilet paper zenye sura yake na T.P hizo zikasambaa maeneo ya
firestation huko Florida.
Ripoti
zinasema toilet paper hizo zimetolewa kujibu mashambulizi baada ya
mfanyakazi mmoja wa kituo hicho cha zimamoto aliziondoa sticker zote
zinazompinga Obama ambazo zilikuwa zimewekwa kwenye maeneo ya umma na
sio maeneo ya watu binafsi ama mali binafsi.
Hata
hivyo toilet paper hizo nazo zimeondelewa maeneo hayo na kupigwa
marufuku maeneo hayo ya Florida firestation kwa sababu ni maeneo ya umma
(public place) na sio maeneo binafsi.
Hivi
karibuni zilisambaa T-shirt zenye maneno ya kumpinga mpinzani wa Barack
Obama katika kinyang’anyiro hicho cha urais wa taifa kubwa duniani Mitt
Romney, t-shirt hizo zilizotengenezwa na vizuri kwa ushirikiano wa
madesigner watatu John Searles, Aaron Rhodan na Julian Streete zina
maandishi yanayosomeka, “That Mitt I Don’t Like.”
Siku
ya jumanne November 6, ikiwa na maana kwamba ni masaa machache tu
kuanzia sasa raia wa Marekani watapiga kura kumchagua rais wa tiaifa
hilo na hapo ndipo maoni ya wengi yatashinda. Ni Romney ama ni Obama
tena?
Kura ndiyo muamuzi wa mwisho, hizi nyingine za kutoleana T-shirt
na kuwekana kwenye toilet paper ni mbwembwe tu na mizuka ya baadhi ya
watu ili kushawishi watu wengine kujiunga nao na kufata maoni yao.