UCHAGUZI WA MAREKANI NI KSHO....OBAMA ANAKIBARUA CHA ZIADA KUTETEA KITI CHAKE CHA URAIS

Wagombea wa urais wa Marekani Barack Obama na Mitt Romney wanaisogelea siku ya uchaguzi huo utakaofanyika kesho kwa kumalizia kampeni zao za mwisho.
Jana Romney alikuwa akizungumza na wapiga kura kwenye jimbo la Pennsylvania ambalo wasaidizi wake wanasisitiza kuwa atalichukua.
Naye Obama alikuwa na mikutano huko New Hampshire na Florida kabla ya jioni kuhutubia kwenye majimbo ya Ohio na Colorado.

Wote Obama na Romney wanakabana koo vilivyo kwa mujibu wa kura za maoni japo kura katika majimbo muhimu zinaonesha Obama kuongoza kidogo.Hata hivyo hakuna kambi iliyo na uhakika wa kushinda hadi sasa.