HAFSA KAZINJA KUTUA BONGO LEO NA ZAWADI YA VIDEO YA "SONGA MBELE"
Malkia wa muziki wa kizazi kipya pamoja na zouk Hafsa Kazinja
anarudi leo nchini Tanzania baada ya kumaliza ziara yake ya miezi mitatu
nchini marekani na leo atawasili Dar-Es-Salaam na ndege ya Shirika la
South African Airline.Kwa mujibu wa Promota wa msanii huyo, bwana Dickson Mkama kutoka
Marekani ametuma taarifa hii kwa watanzania ili wampokee kwa shangwe
pamoja na kumuunga mkongo kwa kile alicho tuletea,
Hafsa aliweza kurekodi nyimbo mpya na mpiga gitaa maarufu kutoka zaire
“NgumaLlokito…na aliweza kufanya video ya wimbo huo na madansa wa
kizungu ambao waliupenda sana wimbo huo unaoitwa “songa mbele”
Aidha promota huyo aliwaomba wapenzi, wadau na mashabiki wa msanii
huyo kujitokeza kwa wingi na kumpokea msanii huyo ambaye ana zawadi ya
video yake mpya ambayo inakwenda kwa jina Songa mbele.