MSANII wa filamu ambaye pia anafanya muziki, Zuena Mohammed ‘Shilole’ na demu mwenzake aliyefahamika kwa jina la Hawa Juma ‘Mama Ayana’ hivi karibuni waliwaacha watu midomo wazi baada ya kugandana kimahaba mbele za watu.
Wakiwa eneo hilo, wawili hao walionekana kuwa karibu sana na lilipofika zoezi la kulishana keki na kufika zamu ya Shilole aliyekuwa MC, Hawa aliweka pembeni ‘stiki’ aliyokuwa akiitumia kulishia watu wengine kisha kutumia mdomo wake kumlisha msanii huyo.