"SIJAWAHI KUTOKA KIMAPENZI NA ‘RAY’ WALA ‘TINO’......"– JACK WA CHUZI


WAKATI tetesi zikidizi kushika kasi mtaani kuwa msanii Jack wa Chuzi, amewahi kutoka kimapenzi kwa nyakati tofauti na wasanii wawili Ray na Tino, sasa ameamua kuzikana tetesi hizo kwa madai kuwa hao wote ni rafiki zake na hakuna ukweli wowote juu ya
ishu hiyo.
Taarifa hizo zimeanza kutoka hivi karibuni zikidai kuwa msanii huyo alitembea na jamaa hao kwa nyakati tofauti huku wenyewe wakiwa hawajuani.

Chanzo kimoja kimedai kuwa wasanii hao hakuna hata mmoja aliyejua kuwa walikuwa wanachanganywa, lakini baadhi ya watu walikuwa karibu na Jack ndiyo walikuwa wakijua ukweli wote juu ya mahusiano hayo.


Mwandishi wetu alimtafuta Jack wa Chuz ili kuweka usawa wa ishu hii naye alidai kuwa hakuna ukweli wowote juu ya taarifa hizo na kudai kuwa watu wanatoa maneno ya uongo wana nia ya kumfanya amalize mwaka vibaya.


“Sijawahi kutoka kimapenzi na Ray wala Tino napenda mashabiki wangu wajue hivyo, watu wanapenda kuzusha maneno ya uongo ili tu kumfanya mtu aonekana mbaya, tunaelekea kumaliza mwaka hivyo sihitaji kuzozana na mtu,” aliongeza.