1. Jacob Stephen
Mwigizaji Jacob Stephen amekuwa na mafanikio makubwa katika kazi zake
ambazo zimekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki baada ya kubeba uhusika
kama inavyo takiwa na kufanya mashabiki wake kuvutiwa na kila kazi
anayoitoa.
JB mwenye umri wa miaka 52 kwa sasa ana miliki kampuni yake ya
Jerusalem Film Company ambayo inafanya vizuri baada ya kuzalisha filamu
zaidi ya 23.
2. Vincent Kigosi
Ray The
Greatest amekubalika na jamii kwa ubora wa filamu zake za mwaka jana
ikiwemo Sister Marry.
Yeye na Brandina Chagula a.k.a Johari waliamua kujiunga na kuanzisha kampuni ya kuzalisha filamu iitwayo RJ Company.
3. Hisany Muya "Tino"
Katika soko la filamu Tino ni actor anayekuja kwa kasi kwenye filamu za
mapigano ama action. Mwaka huu ametisha na filamu yake iitwayo CID.
Hapo awali Tino alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu nia
yake ya kuachana na kuigiza filamu za mapenzi na kuamua kufanya za
action ambazo ameonesha kuziweza.