Ukiongelea wasichana warembo walio kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki huwezi kuacha kumtaja Avril Nyambura wa nchini Kenya.
Ndio maana hivi karibuni brand ya Golden Rome Italian Fair iliamua kumpa deal ya kuwa cover model wa vipodozi hivyo baada ya kuvutiwa na urembo wake.Hivyo ni wazi kwanini Diamond aliamua kusafirihadi jijini Nairobi kwenda kufanya video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Kesho’ na kumchagua Avril awe video girl.
Bila kuficha katika mahojiano na kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Diamond alikiri kuwa uzuri wa Avril ndio uliomvutia hadi kumchagua aonekane kwenye video hiyo.
Hivi karibuni mrembo huyo alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo alikaa kwa wiki nzima na huenda walionana na Diamond na kukubaliana kufanya video pamoja.
Kwa namna nyingi video hii inasuburiwa kwa hamu kubwa ili mashabiki wa wasanii hao wote wawili waweze kuona chemistry yao. We can’t wait.