Meneja Mahusiano wa Vodacom DRC Fanny Kazadi,akifanyiwa mahojiano.
Dar es Salaam 13 Des.
2012 … Waandishi wa
habari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wamevutiwa na mafanikio
yaliyopatikana kutokana na huduma ya M-Pesa nchini na kushangazwa na namna
huduma hiyo ilivyofanikiwa kubadili maisha ya Watanzania.
Timu hiyo ya wanahabari ambao wapo nchini kwa ziara ya
kujifunza namna huduma ya M-pesa inavyofanya kazi wamesema huduma ya kutuma na
kupokea fedha kwa njia ya simu ina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko makubwa
kwa nchi za Afrika ukilinganisha na hali halisi ya uduni wa miundombinu barani
humo.
Waandishi hao wako katika ziara ya siku nne nchini wameyasema
hayo wakati wa ziara yao walioifanya katika makao makuu ya kampuni ya Vodacom
Tanzania, na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kupokea maelezo ya namna
huduma ya M-Pesa inavyofanya kazi.
Kampuni ya Vodacom DRC imeanza kutoa huduma ya M pesa hivi
karibuni ikiwa na mwezi mmoja mpaka sasa.