KITENDO cha mwanamuziki Rihanna kutuma ujumbe mfupi kwenye simu ya mkononi kwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Rapa Drake kumesababisha mtafaruku uliochangia kusitisha uhusiano uliopo baina yake na Chris Brown kwa muda
Kutokana na kitendo hiko wawili hao walionekana kutokuwa na furaha hatimaye wamefikia uamuzi wa kusitisha uhusiano kwa kipindi kisichojulikana
Wawili hao walionekana kuwa na ugomvi katika usiku wa tuzo za Grammy ugomvi uliosababishwa na Rihanna kutuma ujumbe kwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani
Chanzo cha habari kilisema "Rihanna alipokuwa akituma ujumbe huo Chris aliona kitendo chote ingawa hakujisikia vizuri