Tangu matokeo ya kidato cha nne yatangazwe na kuonesha jinsi wanafunzi walivyofeli isivyo kawaida, mijadala kuhusu matokeo hayo imeendelea kushika kasi mitaani, kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii. Kwa upande wake rapper Roma amezitaja sababu 10 ambazo anahisi zimechangia matokeo mabovu ya mtihani wa kidato cha nne nchini.
1. ONGEZEKO LA SHULE ZA KATA
Ongezeko la shule hizi za kata limekuwa kwa kasi sana, lakini shule hizi hazikidhi matakwa ya mwanafunzi kufaulu, hii ni kutokana na ukosefu/upungufu wa walimu/ miundo mbinu ya kufundishia.
Walimu wengi wanashindwa kukabiliana na changamoto zilizopo ktk shule hizi hasahasa huduma mbalimbali kukosekana kwa maana nyingi huwa zipo vijijivi sana, na tunafahamu kuwa vijijini ndiyo tupo wengi kuliko mjini.
Hivyo walimu wengi hushindwa kuwepo kwenye maeneo yao au vituo vya kazi walivyopangiwa, na hii hupelekea ukosefu wa walimu.
2. VIFAA VYA KUFUNDISHIA
Hapa tumekuwa tukilaumu sana MAABARA, tumemsikia waziri jana akisema MAABARA ni tatizo kubwa la kufeli. Sio kweli kwamba ni maabara pekee, kwa maana mbona MATHEMATICS, CIVICS, ENGLISH NA KISWAHILI, GEOGRAPHY etc. havihitaji maabara na wanafunzi wanafeli bado. So tukisema vifaa tujumuishe kwa nguvu moja vile vyote vitumikavyo kufundishia, bado hadi leo kuna tatizo la wanafunzi 7 kutumia kitabu kimoja. Mambo ya head master kufata chaki mjini sikuyatunga tu kichwani, nimeyashuhudia sana.
3. MGOGORO KATI YA WALIMU NA SERIKALI
Kumekuwa na kutoelewana kwa madai ya walimu dhidi ya serikali kwa kipindi kirefu, baada ya serikali kushindwa kutekeleza madai haya imepelekea kushuka kwa ari ya kufundisha kwa walimu.Lakini pia nahisi kama utungaji wa mitihani kwa walimu hawa ulikuwa ni kwa njia ya MKOMOENI(MTIHANI MGUMU) ili serikali ione pengo lake, hali iliyopelekea kuwakomoa na wanafunzi pia.
4. MALIPO DUNI KWA WALIMU
Hii hupelekea mwalimu kujihusisha na shughuli mbali mbali za kumuingizia kipato(ujasiriamali).Sasa kama mwalimu kafungua kibanda chake cha kufuga kuku na kikawa kinamuingizia kipato basi bila shaka ata concentrate na kibanda hicho ilihali akijua mshahara wake wa ualimu uko palepale, so itapunguza kasi ya yeye kufundisha.
5.MAANDALIZI YA MWANAFUNZI(MSINGI)
Wengi hawaandaliwi kufaulu tokea msingi wao, mwanafunzi analazimishwa kungia sekondari wakati hajafaulu darasa la saba, hii inapelekea kushindwa kumudu vitu vingi akiwa sekondari maana hana msingi imara. Namuuliza mwanafunzi wa form two mbili toa tatu(2-3?) ni ngapi? ananitolea macho kisha ananijibu haiwezekani? wakati hiyo ni topic ya darasa la 3/4 au 5.Inabidi nichukue muda wa ziada kumfundisha mambo ya darasa la 5,6,7 ndiyo twende sasa form 1.Huo ni mwaka wa form 3 sasa so anakuwa hamalizi syllabus.
6. WALIPOFUTA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI
Hii iliwafanya wasichujwe na kupata ile cream itakayo weza kupata alama za juu kwa vidato vya mbele ya form two kama ilivyo zamani. Mitihani kama hii humpima mwanafunzi akiwa hatua za awali ili kuweza kumuanda na hatua za mbeleni(form 4).
7. USHINDANI HAKUNA
Siku hizi hakuna ushindani wa kielimu kama zamani, wanafunzi wanashindana mambo mengine tu ya kijamii na sio masomo kama zamani.Globalization inasaidia sana kama wataitumia vema na ipasavyo ila hiyo hiyo inaweza ikawaharibu pia, so hii hupelekea kushindana mambo mengine na kusahau ushindani wa kimasomo.
8. SYLLUBUS
Walimu wanatumia silabasi kufundishia lakini mitihani intoka nje ya silabasi wanayopewa wanafunzi. ( HAPA NAONA WENGI WANAWALAUMU TU WANAFUNZI LAKINI SIONI KAMA WALIANGALIA MITIHANI YAO)
So mwanafunzi inamuwia vigumu maana hana tuition anategemea mwalimu, na mwalimu anategemea syllubus, na syllubus haipo kwenye mitihani, nasoma hiki kinatoka kile nitafaulu vipi?
9. FAMILIA
Familia pia zichangie kuwafundisha watoto misingi bora ya elimu,tatizo lije mzazi / mlezi naye hana elimu hiyo ni changamoto ingine.
10. WALIMU
Walimu hawaandaliwi kuwa walimu bora haswa.Nadhani kwa maana kwa sasa lile ongezeko la walimu siyo kwa ajili ya wito na ndoto zao la hasha. Sio wote wapo hivo!! hii hupelekea wengi kukosa ile taaluma na moyo na wito wa kuweza kudeliver ile knowledge aliyonayo kwa mwanafunzi. Kufundisha ni kipaji unaweza ukawa na akili sana lakini usiwe na uwezo wa kumfanya mwenzio aelewe somo.
WAZO LANGU
Tutazame mfumo mzima wa elimu na sera nzima ya elimu ibadilike kulingana na teknolojia na nyakati za sasa hivi, na kuyasawazisha mapengo hayo hapo juu yote.Dunia inabadilika inabidi tubadilike na sisi katika vingi.Wanaofaulu wamekubali kubadilika wengi wao.Poleni sana waliofeli na hongera kwa waliofaulu.