AY KUTUMBUIZA KATIKA NDANI YA BBA SOUTH AFRICA JUMAPILI HII

Msanii Ambwene Yesaya au ukipenda AY, anatarajia kuwa jukwaani mwisho mwa wiki hii(Jumapili) nchini Afrika Kusini wakati wa Eviction ya washiriki wa Big Brother Africa(BBA)-Star Game

AY anakuwa msanii wa pili kutoka Tanzania kupata nafasi ya kutumbuiza nchini humo wakati wa BBA baada ya Diamond kufanya hivyo wiki chache zilizopita. Lakini hii si mara ya kwanza kwa AY kupanda jukwaa katika Big Brother Africa kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka 2009.

Unaweza kuangalia show ya AY Live wakati wa eviction kupitia DSTv