Mwenge Wa Uhuru Wawasili Mkoani Rukwa


 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Sumbawanga .
Viongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa wakiwa na viongozi wa Wilaya ya Sumbawanga wakikimbiza mwenge katika moja ya barabara za Manispaa hiyo ikiwa ni kuunga Mkono na kukagua mradi wa Sumbawanga Ng'ara ambao lengo lake kuu ni kudumisha usafi katika Mji wa Sumbawanga. Mradi huo umeasisiwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya na kuzinduliwa rasmi na Mhe. Makamu wa Rais Mohammed Gharib Billal alipokuwa ziarani Mkoani Rukwa

 Kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa akiwa anazungumza na wananchi wa Mkoa wa Rukwa. Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru lengo lake kubwa ni kuhamasisha miradi ya maendeleo pamoja na kuubiri amani na mshikamano ambao ndio nguzo kubwa ya mafanikio ya nchi ya Tanzania. Alisema wale wote wanaoipiga vita Serikali iliyopo madarakani hawaitendei haki kwani maendeleo yote yaliyoletwa nayo ikiwemo barabara na mashule wanazitumia wote bila kujali dini zao au vyma vyao.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mathew Sedoyyeka akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya tayari kwa kuanza mbio zake katika wilaya hiyo ambapo baadae utaenda Wilaya ya Kalambo na kumalizia katika Wilaya ya Nkasi.