Nape Akutana Na Walimu Mafinga


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na walimu wa shule za sekondari na za msingi mjini Mafinga mkoani Iringa, leo katika ukumbi wa Southern Highland,  ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaji ilani ya Chama tawala cha CCM mkoani humo. Katika mazungumzo hayo Nape alipata fursa ya kusikiliza kero za walimu na kujadili nao jinsi ambavyo serikali itakavyoweza kuyatatua.


Walimu wa shule za sekondari na msingi wa mjini Mafinga, wakimsikiliza Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipozungumza nao leo kwenye ukumbi wa  Southern Highland mjini Mafinga mkoani Iringa.