Askofu Mdegela Kulipa Milion 50 Endapo Atashindwa Kesi Ya Kumfukuza Mchungaji, Mwingine Ajitokeza Kumshitaki


Mgogoro mkubwa unaolisibu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa sasa utahamia mahakamani baada ya Mchungaji Lambert Mtatifikolo na Mjumbe wa Halmashauri ya Dayosisi hiyo, John Msigomba kufungua kesi mahakamani dhidi ya askofu huyo.
Kwa pamoja Mchungaji Mtatifikolo na Msigomba wanatetewa na wakili Alfred Kingwe wa mjini Iringa dhidi ya mdaiwa wao Askofu Dk Owdenburg Mdegella.

Katika madai yake kwa Askofu huyo, Mchungaji Mtatifikolo anapinga kuvuliwa uchungaji kupitia barua ya Juni 3, 2012 iliyoandikwa na askofu huyo.


Katika mazingira ya kutatanisha na ambayo kisheria hayakubaliki, Mchungaji Mtatifikolo kupitia wakili wake huyo anasema wakati barua ya kuvuliwa uchungaji (nakala tunayo) iliandikwa Juni 3, 2012, kikao cha Kamati ya Utendaji ya Halmashauri Kuu ya Dayosisi hiyo kinachodaiwa kufanya maamuzi hayo kiliketi Juni 27, 2012.


Pamoja na barua ya kuvuliwa uchungaji kuandikwa siku nyingi kabla ya kikao, maamuzi yaliyotolewa kupitia barua ya askofu huyo hayakufuata taratibu kwa kuwa hakupewa fursa ya kujitetea kwa kuzingatia sheria za nchi na sheria za kanisa.


Mchungaji Mtatifikolo anasema maamuzi ya askofu huyo yamemvunjia heshima na anaitaka Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Iringa, imuamuli pia kumlipa fidia ya Sh Milioni 50 kwa kuchafuliwa jina lake.


Kwa upande wake Msigomba anapinga kuondolewa katika nafasi yake ya ujumbe wa halmashauri kuu ya dayosisi hiyo kwa madai kwamba utaratibu uliotumika kufanya maamuzi hayo haukuwa sahihi.


Katika majibu yake kwa Askofu huyo, Msigomba anakiri kupokea barua inayositisha wadhifa wake huo Julai 7, mwaka huu hata hivyo anasema akubaliani na maamuzi hayo kwa kuwa yana dosari nyingi.


Dosari hizo ni pamoja na

1. Wenye mamlaka ya kumuondoa kwenye nafasi hiyo ni wajumbe wa mkutano mkuu wa usharika wake wa kihesa waliomchagua kwa kura nyingi. (Askofu na kamati yake wanaweza kupeleka mapendekezo yao katika mkutano huo na sio kufanya maamuzi).

2. Kama kamati hiyo ilikutana kama invyoonekana kwenye barua aliyopewa, mbona yeye kama mjumbe mtuhumiwa hakuitwa kujitetea kwani yeye ni mfungwa?


3. Barua za kiutendaji zinapaswa kuwandikwa na Katibu wa Dayosisi, sio Askofu wa Dayosisi. Kwanini barua hiyo iandikwe na Askofu?


Msigomba anasema haki yake hiyo ana hakika ataipata mahakamani kwa kuwa dayosisi hiyo hivi sasa inaendeshwa kwa kutumia Nyengo (Kisu kikubwa) na sio kwa kutumia neno la Mungu
Chanzo:http://www.frankleonard.blogspot.com/