Chuji aipeleka Yanga nusu fainali; yailaza mafunzo kwa mikwaju ya Penati 5-3

 
 
MABINGWA  watetezi wa Kombe la kagame leo imefunzi kucheza nusu fainali ya kombe la Kagame kwa kuilaza Mafunzo ya Zanzibar kwa mikwaju 5-3 ya penati baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare 1-1.

Mafunzo wanakila namna ya kujutia mchezo wa leo ambao Said Bahanuzi amefikisha goli la 7 baada ya kufunga magoli mawili moja la kuisawazishia Yanga na lapili katika matuta.

Mafunzo ilikosa penati moja kupitia mchezaji wake Saidi Shaban jambo lililoigharimu timu hiyo iliyoonesha kiwango cha hali yajuu katoka soka hii leo.

Aidha Yanga ambayo awali ilikuwa ikifurahia kupita kilaini katika mchezo waleo nayo itabidi kujifua kikamilifu katika mchezo wake wa nusu fainali hasa kwa washambuliaji wake ambao mara kadhaa walikuwa wakikosa magoli hususani Hamis Kiiza.
 Katika dakika 90 za mchezo Mafunzo kutoka Zanzibar , ili ivimbishia msuli Mabingwa wa watetezi wa Kombe la Kagame, Yanga ya Dar es Salaam kwa kumaliza nao mchezo kwa sare ya 1-1, katika mchezo war obo fainali ya pili ya Michuano ya CECAFA Kagame CUP 2012.

Mafunzo ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza kupitia kwa Ali Othman Mmanga na dakika ya 46 Yanga ilisawazisha g kupitia kwa Said Bahanuzi.
Mafunzo na Yanga zote kutoka Tanzania bara na Visiwani zimechuana katika mchezo wa   wa pili wa robo fainali ya Kombe la Kagame 2012  katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu ya Mavunzo imeonesha kiwango kikubwa cha soka safi huku wakifanya mashambulizi ya mara kwa katika lango la Yanga ambao wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wao wa leo.

Aidha wachambuzi wa soka la Bongo wanatoa tafsiri mbaya kwa Yanga baada ya kumaliza kipindi cha kwanza nyuma ya Mafunzo na kusema kuwa mamechi nyingi za Yanga imekuwa ikishinda katika kipindi cha kwanza.