JENIFER AWAASA WAZAZI KUWA MAKINI NA WATOTO.

Hanifa Daud
 
 Jenifer akiwa katika pozi la picha.
MWIGIZAJI mtoto mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jenifa Daudi ‘Jenifer’ amesema kuwa kuna baadhi ya filamu zinazotengenezwa hapa nyumbani hazistaili kuangaliwa na watoto hata kushiriki kuigiza kwa sababu zinapotosha watoto kulingana na vitu vinavyoonyeshwa katika filamu hizo, akisema kuwa filamu hizo ni za kikubwa sana.“Sisi ni watoto wadogo ambao tunataka kujifunza mambo mazuri kutoka kwa wakubwa kama watoto lakini kuna filamu wameshiriki watoto na ni mbaya, Uncle Kanumba alikuwa akitengeneza filamu za watoto nzuri ambazo zimeniletea sifa mimi na watoto wezangu na kila mtu anatupongeza kwa filamu zile,”anasema Jenifer.
 
Jenifer alitolea mfano wa filamu ya House Boy ambayo imetengenezwa na kutoka hivi karibu akisema kuwa filamu hiyo haifai kwa kutazamwa na watoto kwani ina mambo ya ajabu sana huku ikiwa imeigizwa na mtoto mwenzao ambaye ni Lulu, Jenifer amewasisitiza wazazi kuwa makini na watoto katika kushiriki filamu pia kujua ni filamu zipi wanatakiwa kuangalia