Mwigizaji,Zuwena MohamedMWANADADA mwigizaji na mwanamuziki, Zuwena Mohamed Shilole, amesema baada ya kujiongezea fani nyingine na kufanya vizuri ni kama kafungua njia kila mwigizaji wa kike anataka kuimba japo hawana uwezo huo.
Anasema kuwa wanapoona Shilole anakataa viuno wanajua kuwa kila msanii atakata viuno tu na kuwa mwanamuziki mkali.
Nawapa pole wenzangu toka nimefungua njia na kuanza kuimba naona watu wanakurupuka na kuingia katika fani ya uimbaji, sikukurupuka nilijipanga kwa ajili ya kazi na kazi inaonekana," anatamba.
"Napata shoo ambazo hata wasanii wakubwa hawapati, mimi si kama hawa wakataa viuno wanaoiga tu baada ya kumuona Shilole, sifanyi maigizo nafanya kazi inayokubalika katika jamii."
Shilole anasema muziki na filamu vinampatia kipato na kuweza kuwasomesha watoto wake wawili katika shule ya kimataifa, kuendesha gari zuri na kuishi nyumba nzuri pia.
"Kwangu filamu na muziki ni biashara," anasema.
Shilole pia amekamilisha nyimbo nyingine alizoimba kwa kuwashirikisha wasanii Mzee Yusuf (Kachumbari), Barnaba (Surprise), Q Chilla (Dudu) na Richi Mavoko na Kitokololo (Viuno).