ADEBAYOR MBIONI KUSAINI MKATABA WA KUDUMU SPURS.

 


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor anakaribia kusaini mkataba wa kudumu na klabu ya Tottenham hotspurs mkataba ambapo utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo. Inaaminika kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu ambao utamuwezesha kulipwa kiasi cha paundi 115,000 kwa wiki na kuongezewa kiasi cha paundi milioni nne kama motisha. Mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko naye anaweza kumfuta Adebayor katika wachezaji ambao wataondoka katika klabu hiyo msimu huu baada ya AC Milan kuonyesha nia ya kumsajili katika kipindi hiki cha kiangazi. Spurs pia wamekuwa wakihitaji kumsajili beki wa klabu ya Nottingham Forest Jamaal Lascelles kwa ada ya paundi milioni 5.