Mtuhumiwa
wa wizi wa umeme,Bi Siwamini Muhammed akitoa maelezo kwa wakagazu wa
umeme na askari kabla hawajamchukua na kwendanae kituo cha polisi Kilwa
Road.
Mtuhumiwa
wa wizi wa umeme Siwamini Muhammed, akiwa chini ya Ulinzi wa jeshi la
polisi na wakaguzi wa Shirika la umeme Tanesco baada ya nyumba yake
ilioko Mbagala kizuiani kukutwa ikiwa imeunganishwa umeme kwa njia ya
wizi kabla haujafika kwenye mita nakuutumia bila kuulipia.
Askari akitimiza wajibu wake wa kuwalinda watuhumiwa wa wizi wa umeme waliomo ndani ya gari kabla ya kuwapeleka kituoni.
WATU
saba wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi wa umeme
baada ya kuwakamata kwenye operesheni ya kukamata watu wanaoiba umeme
inayoendelea kwenye kanda maalum ya Tanesco Temeke.
Kwenye
zoezi hilo ambalo linafanywa na timu maalum ya Tanesco na kusaidiana
na Jeshi la Polisi kumegundulika wizi wa aina mbalimbaliikiwemo
wakujiunganishia umeme kwa kupitisha waya chini ya aridhi na
kujiunganishia kabla haujafika kwenye mita na kusomwa.
Zoezi
hilo ambalo jana ilikuwa ni zamu ya eneo la Mbagala Kizuiani liliwapa
wakati mgumu wakaguzi wa mifumo ya umeme wa shirika hilo baada ya
kufika mtaa wa CCM eneo hilo la kiuzuiani na kukuta nyumba zaidi ya 6
wakitumia umeme kutoka kwenye nyumba moja huku wakiwa wamejiunganishia
kwa kuchumbia nyaya chini ya aridhi na wakaguzi hao kuamua kukata kabisa
waya zake na kuwashikilia watuhumiwa wa wizi huo.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo Meneja wakanda hiyo ya Temeke Richard Malaamia,
amesema tatizo la wizi nikubwa kwahiyo wanalazimika kufanya zoezi hilo
kuwa endelevu hadi wananchi watakapojenga mazoea kutumia umeme kwa
kufuata utaratibu.
Malamia amesema wisi wa umeme uekua ukisababisha hasara ya Tsh 89Millioni kwa mwezi na kulikosesha mapato shirika hilo.
Hata
hivyo wakaguzi wa mifumo ya umeme walimweleza mwandishi wa habari hizi
kuwa wao binafsi walidhani tatizo la wizi wa umeme lipo zaidi kwa
watumiaji wakubwa lakini kkutokana na matukio wanayoshuhudia inawapa
wasiwasi kuwa kuna idadi kubwa zaidi ya watu wanao iba umeme hata kwa
watumiaji wadogo kabisa.
Mkaguzi
Daniel Maswi alisema, tabia ya kujiunganishia umeme kabla ya kufika
kwenye mita ni hatari na inaweza kusababisha hatari hata ya kulipua
nyumba kwani nyaya zinazo tumika ni hafifu mno na umeme unaopita ni
mkubwa.