Tarehe
11/07/2012 Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
iliwasilli nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi. Kamati hiyo uliyongozwa
na Mwenyekiti wake Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Edward Lowassa
aliyefuatana na wajumbe wengine ambao ni Mhe. Beatrice Shelukindo,Mhe.
Rachel Mashishanga, Mhe. Vita Kawawa, Mhe. Khalifa M. Khalifa na Bw.
Ramadhani Issa Abdalla ambaye ni Katibu wa msafara.
Tarehe
12/07/2012, kamati ilitembelea bunge la Uingereza na kupata uzoefu wa
namna bunge hilo linavyoendesha shughuli zake. Aidha Kamati ilitembelea
nyumba na mali zinazomilikiwa na serikali ya Tanzania nchini
Uingereza.
jana
tarehe 13/07/2012 kamati ilitembelea ofisi ya Ubalozi na kuzungumza na
Maafisa wa Ubalozi. Kupitia mazungumzo hayo, Kamati ilifanikiwa kusikia
shughuli za ubalozi, mafanikio na changamoto mbalimbali zilizopo
katika utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya Uchumi nchini Uingereza.
Aidha Kamati ilipata nafasi ya kutembelea taasisi maarufu
inayojishughulisha na masuala ya sera za kimataifa ya CHATAM HOUSE na
kuelezea sera za Tanzania katika masuala ya siasa za kimataifa na
uchumi.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mbunge wa Monduli na ambaye ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mh. Edward
Lowassa(nne kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mh. Peter
Kallaghe(tano kushoto), wakiwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Bunge.
Kutoka kushoto , Mh. Rachel Mashishanga, Mh. Beatrice Sherukindo, Mh.
Vita Kawawa, Mh. Khalifa M Khalifa(tatu kushoto), Naibu Balozi, Mh.
Chabaka Kilumanga na Katibu wa Msafara
Pichani,
Mheshimiwa, Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu), akiwa katika picha
ya pamoja na Balozi, Wajumbe wa Kamati na Maofisa wa Ubalozi.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Lowassa akisindikizwa na Mheshimiwa
Balozi Peter Kallaghe na Maofisa wa Ubalozi baada ya kumaliza mkutano na
Maofisa wa Ubalozi. Picha na Allly Rashid Dilunga