Rais John Atta Mills wa ghana afariki Dunia leo hii

Habari za Uhakika zimeifikia blog hii kuwa Rais John Atta Mills wa Ghana, amefariki dunia jana jumanne 24 julai 2012 mjini Accra,Ghana.
Umati wa maelfu ya watu mapema jana walikua wamezunguka katika hospital ya jeshi ya   37 Military Hospital iliyopo mjini Accra.

Marehem Rais John Atta Mills (68) alifariki jana mapema baada ya kupelekwa katika  hospital hiyo ya kijeshi,mpaka sasa haijulikani ugonjwa gani ulikua unamsumbua.

Taifa hilo la Ghana linakumbwa na msiba huu wakati wakielekea katika uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Desimba mwaka huu.
Mungu amlaze pema peponi Rais John Atta Mills(RIP).