MASHABIKI WA SIMBA:HUU SI UUNGWANA WALA UPENZI WA MICHEZO

 
 Mashabiki wa Simba, jana wamemtembezea kichapo mama mmoja aliyekuwa amevalia jezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars yenye nembo ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), kosa kukaa kwenye jukwaa walilokuwa wamekaa wao.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Sasa haikuweza kufahamika mara moja, mashabiki wa Simba wana bifu na TFF au hawapendi timu ya taifa. Mama huyo alikimbizwa huku akipewa kichapo hadi kutokwa damu, kabla ya kuokolewa na Polisi waliomteremsha jukwaani. Aliporwa vitu vyake kama pochi na kadhalika.

Baadaye akiwa amekwishaokolewa na askari, ndipo msamaria mwema mmoja, albino akamuokotea baadhi ya vitu na kuwakabidhi askari. Huwezi kulipa jina lingine tukio lile, zaidi ya udhalilishaji wa kijinsia. Alikuwa anatia huruma mama huyo wakati anahangaika kujitoa kwenye kundi la mashabiki wa kiuma wa Simba, iliyofungwa 3-1 na Azam  katika Robo Fainali ya Kombe la Kagame.
Picha na Habari Kwa Hisani ya Bin Zubery wa BongoStaz.Blog