Mbali na wasanii hao wa Marekani pia Belly 9 alisema kuwa ameshafanya collabo nyingine na wasanii kama Nazizi kutoka Kenya na Cannibal huku akiamini kuwa kuvuka mipaka ya kufanya kazi na wasanii hao kunaweza kufungua njia nyingine ya kufika mbali zaidi.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na ngoma nyingine mpya inachokwenda kwa jina la ‘Anayeishi naye’, ambayo ndani yake anapatikana kijana Ben Pol, wakati ngoma zake kama ‘Amerudi’, ‘Suma ya Penzi’, ‘Masogange’ bado zinafanya vizuri.
“Malengo
yangu ni kutoka kimataifa kwani nafanya muziki ili nao uniweke
kwenye nafasi fulani kimaisha, muziki ni ngumu pale unapoufanya kama
mchezo lakini unakuwa mzuri pale unapoufanya kwa malengo na kujua ni
kazi hivyo kwa upande wangu nalenga kufika mbali zaidi,” alisema.
Hata
hivyo aliongeza kuwa hana mpango wowote wa kutoa albamu kwa mwaka huu,
kwani tatizo kubwa linalomuumiza ni pale watu wanapotumia njia za
mkato kama ku-burn albamu ya msanii huku wakisahau kuwa wao wanatumia
gharamu nyingi za pesa na muda katika kutengeneza wimbo hadi unakuja
kukamilika na kwenda sokoni.