MWIGIZAJI
wa filamu mwenye jina kubwa , Amanda Poshi amefunguka kuhusu
kutalikiana na aliyekuwa mumewe Hamis Bwela ambaye aliachana naye siku
za karibuni kutokana na sababu ya mumewe kumzuia asifanye kazi yoyote
zaidi ya kukaa ndani tu na kama akitoka wawe sote.
Amanda amedai kuwa mumewe alipomuoa alijua kuwa yeye ni mwanamke mjasiriamali ambaye pamoja na kufanya shughuli zake ndogo ndogo lakini kazi yake kubwa ni uigizaji ambayo anaamini kuwa inawezekana hata mumewe huyo alimwona kupitia filamu na tamthilia na kumpenda awe mkewe iweje amzuie asifanye kazi yoyote?
Amanda Poshi
“Ndoa
imenishinda aliyekuwa mume wangu alikuwa hataki kabisa nifanye kazi
yoyote zaidi ya kukaa ndani tu, maisha ya sasa si maisha ya kusubiri
uletewe kila kitu lazima mwanamke uhangaike na si kuwa tegemezi sasa
mtu ukae ndani tu kama mwali au mwanamke wa mwarabu maisha ya sasa,”anasema Amanda.Amanda amedai kuwa mumewe alipomuoa alijua kuwa yeye ni mwanamke mjasiriamali ambaye pamoja na kufanya shughuli zake ndogo ndogo lakini kazi yake kubwa ni uigizaji ambayo anaamini kuwa inawezekana hata mumewe huyo alimwona kupitia filamu na tamthilia na kumpenda awe mkewe iweje amzuie asifanye kazi yoyote?