SHILOLE AGWAYA KUMTAMBULISHA MPENZI WAKE KISA KIKIWA NI KUHOFIWA KUPORWA....!!!


STAA wa filamu na muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameiambia jicholetu  kuwa anaogopa kumtambulisha kwa mashosti zake bwana’ke aliyenaye kwa sasa akihofia kuporwa.

Shilole anayedaiwa kunasa kwenye penzi la mtangazaji, alisema kuwa anaogopa kumweka hadharani kwani kuna baadhi ya wasichana wa mjini wakishamjua mwanaume wa mtu, huwa wanamnyemelea na kumnasa kirahisi, jambo ambalo hataki limtokee.