Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya
almaarufu kama Bongo fleva juzi usiku walikwenda mpaka Kibaha mkoani
pwani katika Studio za Usanii Production na kufanya kolabo ambayo
ilichukua zaidi ya masaa manne kukamilika na kupewa jina la Boda Boda.Kolabo hiyo ambayo imesimamiwa na
Produza mahiri Fundi Samweli na wasanii hao wawili wenye staili mbili
tofauti inasemekana kuwa itakapotoka itakuwa kali sana baada ya wadau
waliokuwepo wakati kolabo hiyo ikifanyika kutonya kwamba ina viwango
vya juu kwani wasanii wote wawili wamejitahidi kufunikana kuanzia
sauti, utunzi na ujumbe.
“Kaka shughulu ilikuwa pevu studio kwani wasanii wote wawili walifika studio mida ya jioni na kuanza kujipanga kwa takriban masaa mawili baada ya hapo walienda ndani na kuanza matayarisho ya mwisho kabla ya kuingiza sauti mida ya usiku sana". Tunamnukuu mdau John Anthony aliyekuwepo maeneo ya studio siku ya jumatatu jioni mpaka usiku