Mangula Makamu Mwenyekiti Mpya CCM

Chama Cha Mapinduzi kimemteua Katibu Mkuu wake mstaafu, Philip Mangula kugombea nafasi ya Makamu Mwemnyekiti wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara huku kwa Zanzibar akiteuliwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.Uteulzi wa wagombea hao umefanywa na Kikao Cha CCM na Kuthinishwa na NEC usiku wa kuamkia leo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema leo mjini Dodoma.

Mangula na Dk. Sheni watapigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu, unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Kizota nje kidogo ya mji wa Dodoma.