MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, ameangua kicheko baada ya kusikia mwigizaji Irene Uwoya kunaswa hotelini na Nasibu Abdul ‘Diamond’. Jokate aliangua kicheko hicho juzikati jijini, Dar wakati alipozungumza na paparazi wetu na alipogusiwa kuhusu suala la Uwoya kunaswa na Diamond, alicheka sana huku akimshangaa. “Hahaha sasa ndiyo nini tena, yeye si aliwahi kunisema mimi nakwapua mabwana? Sasa leo imetokea kwake tena!” alisema Jokate.