KAJALA, LULU NI MUNGU TU


IMEBAINIKA kuwa wasanii wawili maarufu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Kajala Masanja ambao sasa wako katika matatizo wakikabiliwa na tuhuma mbili tofauti sasa wamemgeukia Mungu.
Chanzo chetu ndani ya Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam walikofungiwa wasanii hao zinasema mara baada ya kukutana gerezani na kuombewa na waumini wa Kanisa la Efatha wamekuwa wakishinda wakisoma Biblia.


Habari zinasema licha ya kusoma kitabu hicho kitakatifu kwa waumini wa Kikristo, wasanii hao wamekuwa wakivaa rozali wakati wote badala ya cheni za dhahabu ambazo walikuwa wakivaa walipokuwa uraiani.
“Hivi sasa wamekuwa wakining’iniza rozali shingoni badala ya kuvaa mikufu ya dhahabu, na wamekuwa wakisoma sana Biblia wakiamini kuwa Mungu atawasaidia katika matatizo yao, hakika nakuhakikishia kuwa sasa wamebadilika sana,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilifanikiwa kwa nyakati tofauti kuwaona wasanii hao wakiwa wamevaa rozali hivyo kuthibitisha kilichosemwa na chanzo chetu.

chanzo:http://www.globalpublishers.info