EURO 2012: ITALIA NA SAFU YA USHAMBULIAJI YA WENDAWAZIMU CASSANO NA BALOTELLI.

Maneno ya Cesare Prandelli alipomrithi Marcello Lippi kama kocha wa timu ya taifa baada ya kombe la dunia mwaka 2010 ni kwamba ataifanya Azzuri ivutiwa kwa kucheza soka zuri la kushambulia. Kwa hakika amejitahidi sana huku akitambulisha utaratibu wa 'ethical code' (wachezaji wanaokuwa wamesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu hawatoitwa timu ya taifa) na kusisitiza katika kuwapa nafasi zaidi viungo wenye ufundi zaidi katika timu yake. Wazo ni kuifanya Italia kucheza kwa staili yake ya mfumo wa tiki-taka, staili inayopendelewa zaidi na Wahispania.

Akiuacha mfumo wa siku nyingi wa kujenga ukuta wa chuma na kucheza kwa mashambulizi ya kushtukiza kwa ajili ya mfumo ambao unatumia na Spain, ambao mpaka sasa umeleta matokeo ya mchanganyiko. italy haikufungwa hata mechi moja kwenye hatua ya kufuzu, lakini wamekuwa wakifungwa kwenye mechi za kirafiki. Skendo ya upangaji wa matokeo ambayo inaliandama soka la nchi hiyo kwa miaka mingi sasa, haitegemewi kuwa na madhara makubwa sasa hivi kuliko ilivyokuwa katika miaka 1982 na 2006, sababu kubwa ni kwa kuwa ni wachezaji wachache wa kikosi cha sasa wameguswa na kashfa hiyo, lakini suala hilo bado linabakia kuwa sio zuri kwa wachezaji.
Droo ya group C haikuwa nzuri kwa Italy, lakini atleast mechi yao dhidi ya Spain itakuwa ya kwanza. Na kupata pointi kutoka kwenye mechi hiyo ni jambo ambalo linawezekana, kwa kuangalia Spain huwa na kawaida ya kuanza vibaya michuano mikubwa, ukiangalia kombe la dunia lilopita walipofungwa na Uswis katika mechi ya kwanza makundi. Baada ya mechi hiyo atleast kidogo mambo yanaweza kuwa mazuri dhidi ya Croatia na Ireland.
WACHEZAJI MUHIMU
Gianluigi Buffon
Nahodha amerudi kwenye kiwango chake baada ya majeruhi yaliyomkumba msimu wa  2010-11. Ukifikiria namna safu ya ulinzi ilivyokuwa dhaifu, Azzuri wanahitaji kuwa na Buffon mwenye kiwango cha juu ili kuepeuka balaa. Ni uchizi sasa kufikiri kwamba safu ya ulinzi ambayo siku zote imekuwa ndio nguzo ya timu ya taifa ya Italia, sasa hivi ndio ulipo udhaifu wao, lakini hapa ndipo tulipo, na sasa tumaini lote lipo kwa Buffon na mikono pamoja na miguu yake kutatua hilo tatizo.
Mario Balotelli
Mario Balotelli alisema hatoshangilia goli mpaka atakapofunga goli la ushindi kwenye world cup au Euro, hivyo hii ndio nafasi pekee kumuona Super Mario akicheza kwa furaha baada ya kutupia kambani. Tuache utani, huu ni muda wake kuweza kuonyesha kwanini makocha wamuamini na kumpa nafasi. Balotelli ana nguvu, ujuzi na kimo kizuri, Anachohitaji ni kutulia na kutumia vizuri nafasi atakazopata huku akijiepusha na suala la nidhamu mbovu. Akifanikiwa kwenye hayo atatisha.
Daniele De Rossi
Katika kiungo ambacho kimejaa wapiga pasi mafundi zaidi, De Rossi ndio kiumbe anayetegemewa kusambaza minguvu yake. Shujaa huyu wa Roma ndio sasa anaelekea kwenye kilele chake, akiwa ameshaji-commit kwenye klabu yake, sasa yupo huru kufikiria timu ya taifa tu. Atakuwa na shughuli ngumu katika kupambana na kuizuia safu ya ulizni wa timu ambayo ni dhaifu kutoguswa

 JE SAFU YA USHAMBULIAJI YA MACHIZI ITAFANYA VIZURI?
Mara tu Giueseppe Rossi alipoumia, mikono ya Prandelli ilikuwa imefungwa. Akawa hana chaguo lingine zaidi ya kuwatumia Balotelli na Antonio Cassano. Hii haihusu suala la uwezo  - -wachezaji wote wawili wana vipaji vikubwa tataizo ni nidhamu: wote wawili wana matukio mengi ambayo yanahusu ukosefu wa nidhamu na tabia nyingine tofauti,ndani na nje ya uwanja. Hivyo hilo ni tatizo ambalo Prandelli inabidi alitafutie suluhisho.