Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Moses Nnauye, amesema wanaokihama chama hicho kwenda upinzani ni vinyago, ambavyo kamwe haviwezi kumtisha mchongaji, huku akisisitiza kwamba waasisi wa vyama vya Chadema, NCCR, CUF, TLP na vinginevyo vyote, ambao walikuwa ndani ya CCM miaka 20 iliyopita, wote hawawezi kuitisha CCM. Nape ametoa kauli hiyo wakati akiwahutubia wakazi wa Makambako mkoani Njombe.
Hii ni kauli ya pili ya Nape ndani ya wiki moja, kwani hivi karibuni alisikika akiwaita hao wanaohama CCM kuwa ni Oil Chafu ambayo haina budi kuondolewa kwenye injini ili kuweka mpya.
Chanzo ni taarifa za habari za ITV na TBC1