KAGAWA AKATAA JEZI NAMBA 7 OLD TRAFORD.

 
KIUNGO mpya wa klabu ya Manchester United Shinji Kagawa amepania kufanya vizuri katika klabu hiyo ya Old Traford baada ya kuhamia akitokea klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani.

Kagawa mwenye miaka 23 alikuwa akiwindwa na vilabu vingi duniani baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu msimu uliopita akiwa na Dortmund hatahivyo alikuwa alikuw ana Sir Alex Ferguson ndiye aliyefanikiwa kuipata saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Japan. Mchezaji sasa amepania kuanza upya na kusisitiza kuwa anataka atengeneze jina lake mwenyewe akiwa na klabu hiyo baada ya kukataa kuvaa jezi namba saba aliyopewa ambayo imewahi kuvaliwa na nyota kama George Best, David Beckham na Cristiano Ronaldo. Kagawa mbali na waandishi wa habari waliokuwepo pia alipokewa na mamia ya mashabiki wa klabu hiyo ambao walikuwa wakitaka saini yake na wengine kutaka kumshika mkono. Kuna tetesi kuwa kagawa anaweza kuvaa jezi namba 8,26 au 29 ambazo alikuwa akivaa wakati akiwa katika klabu ya Cereno Osaka ya nchini kwake au namba 23 ambayo ndiyo jezi aliyokuwa akivaa akiwa Dortmund.