Tofauti na website za wasanii wengine nchini, yake Diamond tunathubutu kusema ndio personal website pekee inayoongoza kwa kuwa updated kila siku kwa matukio mapya. Diamond si mwandishi wa habari lakini anajua kuwa yeye ni mtengeneza habari (newsmaker). Katika uandishi wa habari yeye yupo kwenye ule ubora wa habari (news values) ambao kitaaluma unajulikana kama ‘Prominence’.
Yeye ni mtu maarufu kwahiyo chochote anachokisema ama kukiandika sehemu ni habari kwakuwa ni mtu maarufu. Hivyo ana mengi anayoyaandika kwenye website yake yanayotokana na kile akifanyacho kila siku, bila kusahau picha nzuri na nyingi ambazo huziweka mara kwa mara awapo kwenye ziara zake.
Hakuna show anayoenda na asichukue picha za kuja kuwaonesha mashabiki wake. Hakosi la kuandika kuwajuza mashabiki.
Kwanini tunasema wasanii wengine waige mfano wa website yake? Kwanza wasanii wachache ambao wana website ama blog zao wakumbuke kigezo hicho kuhusu ubora wa habari kuwa wao ni ‘newsworthy’ yaani wanatengeneza habari kwa mengi wanayosema ama kufanya.
Ni jambo la ajabu website ya msanii mkubwa inakuwa updated mara moja kwa mwezi tena kwa habari ya ajabu ajabu tu na wakati mwingine haimhusu yeye mwenyewe! Personal websites/blogs zinapaswa kutoa kwa asilimia kubwa habari kuhusu msanii mwenyewe.
Wasanii wengine wamezigeuza personal blogs zao kama blogs zingine za kawaida zinazotoa habari za watu wengine. Diamond anapaswa kusifiwa kwasababu website yake inamuangaza yeye zaidi. Wapi ameenda kufanya show, amekutana na nani, ana mipango gani n.k.
Ukiwa mtembeleaji mzuri wa website yake utayafahamu hayo. Iweje website binafsi ya msanii mkubwa nchini ijae mambo ya watu wengine tu wakati yeye mwenyewe kila siku kuna mambo anayoyafanya na ambayo kama angeyaandika kwa kuambatanisha na picha mashabiki wake wangefurahia!!
Hivyo wasanii wanaomiliki website/blog binafsi watambue kuwa sio fashion kuwa na website ambayo hubadilishwa habari mara moja ama mbili kwa mwezi. Huna haja ya kuwa na website binafsi wakati huna la kuandika. Inabaki kuwepo tu bila kitu chenye kumrudisha tena msomaji.
Kwa wale ambao hawana website/blog zao ni muda mzuri wa kufikiria kuwa nazo. Ni njia nzuri ya kujitangaza. Waandishi wa habari huzitumia kupata habari halisi na zenye ushahidi kutoka kwa msanii husika. Kumiliki tu akaunti ya Facebook na Twitter hakutoshi.