Jana mshiriki wa Kenya kwenye mashindano ya Big brother Africa Prezzo alikuwa akizungumza na mwenzie Talia na kumwambia jambo ambalo limewashtua wengi.
Prezzo ana mpango wa kuomba kutoka kwenye shindano hilo kwa hiari leo.
Sababu za kujitoa anasema ni kutengwa pamoja na kusongwa na hisia kali za upweke ambazo zimemshinda kuzihimili kiasi cha kumfanya rapper huyo kukataa tama ya kuendelea kuwania kitita cha dola laki tatu.
Mwanzoni Talia alidhani Prezzo alikuwa anatania tu lakini baadaye alikuja kugundua kuwa rais huyo CMB yupo serious na alichokisema.
Katika maongezi hayo Prezzo alisema: “My tank is on empty right now. I’m done. I feel so lonely and the isolation is getting to me.” Hata hivyo Talia alimwambia Prezzo kuwa haiwezekani akate tama sasa hivi ambapo wanaelekea mwishoni. ‘Utakuwa ni uamuzi wa kijinga kwako. Fikiria watu wote utakaowaangusha,” alisema Talia.
Ingawa Prezzo alidai kuwa hakuumia baada ya Goldie kutoka kwenye mashindano hayo, kauli yake hii inaashiria kuwa alidaganya. Tangu Goldie atoke kwenye jumba hilo amekuwa hana mtu wa karibu kama alivyokuwa akiishi na Goldie.
Kama kweli akiendelea kuwa na msimamo huo wa kutaka kujiondoa kwenye shindano hilo, Prezzo atawaumiza wakenya wanaomtegema na hata watanzania ambao wamekuwa wakishiriki katika kumpigia kura ili aendelee kubaki.
Wengi watamshangaa kushindwa kuumaliza mkia wakati amemshala ng’ombe mzima kwakuwa zimebaki siku 16 tu hadi kufikia mwisho wa Big Brother Africa Stargame.