TAMASHA LA WAZI LA FILAMU TANZANIA LAZINDULIWA JIJINI TANGA

 Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Tamasha la Wazi la Filamu za Kitanzania maarufu kama Bongo Movie linalodhaminiwa na Kinywaji cha Grand Malt,Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini,Mh. Halima Dendego (katikati) akijiandaa kubonyeza kitufe chenye kuashiria uzinduzi Rasmi wa Tamasha hilo kwenye Viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Tamasha la Wazi la Filamu za Kitanzania maarufu kama Bongo Movie,Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini,Mh. Halima Dendego akiwahutubia wapenzi wa Bongo Movie waliofurika kwa Wingi kwenye Viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga kushuhudia Tamasha la Wazi la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie).Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah na kulia ni Meneja wa Kinywaji hicho cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha hilo,Consolata Adam.
Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na Habari kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Godfrey Mngereza akizungumza machache kwenye Uzinduzi huo.
Meneja Masoko wa TBL,Fimbo Butallah akizungumza machache na wapenzi wa Bongo Movie waliokuja kwa wingi kwenye uzinduzi wa Tamasha la Wazi la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) katika Viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Mh. Halima Dendego na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,Mh. Mboni Mgaza.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Mh. Mh. Halima Dendego akipena mkono wa Pongezi na Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam mara baada ya kufanyika kwa Uzinduzi wa Tamasha hilo.
Burudani ya Ngoma toka kwa kundi la Negro Camp.
Msanii wa Bongo Movie,Richie Mtambalike akionyesha umahiri wake wa kusakata ngoma.
Sebene limekolea hapa
Vijana wa IceCream Dancers wakifanya vitu vyao
Taarab pia ndani.
Salamu Meza Kuu.
Dua ya Kumuombea Marehemu Steven Kanumba.
Wasanii wa Bongo Movie.
Nembo ya Tamasha.
Toka kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti,Mafunzo na Habari kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Godfrey Mngereza,Meneja Mauzo wa TBL,Fimbo Butallah,Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Mh. Mh. Halima Dendego,Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,Mh. Mboni Mgaza na Mwisho ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam.