Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 "Bhaasi"
Bwana Sebastian Maganga akiwapongeza washindi wa Serengeti Fiesta Super
Nyota Super J. kulia na Neylee, mara baada ya wasanii hao kuibuka
washindi katika shindano hilo lililofanyika usiku huu kwenye klabu ya
Vibes jijini Mbeya, wasanii hawa watauwakilisha mkoa wa Mbeya katika
matamasha mbalimbali ya Serengeti Fiesta mikoani
Mtangazaji wa Clouds Antu Mandoza akizungumza jambo mara baada ya
kuwakabidhi zawadi zao za kreti mbili za bia aina ya Serengeti Lager
kutokana na ushindi wao katika shindano hilo lililomalizika usiku hu
jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Bw. Sebasttian Maganga akitangaza washindi katika shindano la Serengeti
Fiesta Super Nyota lililomalizika usiku huu kwenye klabu ya Vibes jijini
Mbeya.
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kwenye klabu ya Vibes ili kushuhudia
shindano hilo wakifuatilia kwa makini wakati wasanii hao walipokuwa
wakishindana.
Msanii Super J. akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki waliojitokeza katika klabu ya Vibes usiku huu.
Msanii 1 Rich akionyesha uwezo wake jukwaani wakati wasanii wa muziki wa
kizazi kipya Bongofleva waliposhindana kuimba katika shindano la
Serengeti Fiesta Super Nyota lililomalizika usiku huu kwenye klabu ya
Vibes jijini Mbeya
Mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wakiwashangilia wasanii walipokuwa
wakishindana katika shindano la Serengeti Fiesta Super Nyota.
Kutoka kulia wa pili ni Shafii Daudam Sebastian Maganga na Antu Mandoza
wakifurahia jambo pamoja na mshabiki wengine waliohudhuria katika
shindano hilo.
Mashabiki wapata burudani ya muziki kabla ya kuanza kwa shindano hilo.