Rita Paulsen |
Mitandao ya kijamii hususan Facebook na Twitter, huonesha kirahisi namna watu maarufu wanavyokubalika zaidi kwa mashabiki.
Kuna
nyota wengi Tanzania ambao pamoja na umaarufu wao mkubwa hawana
ushawishi wowote kwa mashabiki wanaowafuata Twitter au kulike page zao
za Facebook.
Usishangae
unapoona nyota ana mashabiki zaidi ya 20,000 Facebook lakini aandikapo
kitu comments hazizidi 100. Unadhani kwanini iko hivyo? Ni kutokana na
jinsi mtu huyo alivyo na ushawishi mkubwa.
Kwa
Utafiti tuliyoifanya Facebook, tumebaini kuwa katika nyota wa Tanzania
ama watu watu maarufu ukiachana na wale waliopo kwenye siasa, Rita
Paulsen aka Madam Rita wa BSS, ndio mwanamke, nyota wa Tanzania mwenye
ushawishi mkubwa kuliko wote Tanzania. Je! ni kwasababu ya uzuri wake?
Chochote
aandikacho, hata kama ni cha kawaida tu, hupata maoni mengi tofauti na
status za watu wengi kwenye kurasa za Facebook ambao wanamzidi hata
idadi ya mashabiki waliolike page zao.
Anafuatiwa na Lady Jaydee na Fid Q. Huu ni mfano wa status zao na jinsi zinavyochangiwa.
Madam Rita
19.08.2012
Nawatakia mashabiki wangu wote Eid njema. Eid Mubarak!
Comments – 218, likes 413
21.08.2012
Ahsanteni sana kwa support mlionionyesha na mnayo endelea kunionyesha kipindi hiki cha matatizo. Nawatakieni siku njema.
Comments – 425, likes 644
24.08.2012
Hamna utajiri mkubwa duniani kama afya yako. Nawatakia Ijumaa njema.
Comments 178, Likes 429
Lady Jaydee
Julai 21, 2012
Good
morning, kuna siku ningependa nikutane na wote nyie mlioko humu ndani
ila sijui nitafanyaje, na itakuwaje?? Mko kama 14,953 au ningoje mfike
15,000 tukutane kwa namba ya 100 mia?? Let me know
Comments 228, likes 333
Julai 30
STATUS
zangu hazihusiani na STORY za magazeti, poleni kwa mlioelewa vibaya
ila ni mgongano wa mawazo, kuna mtu kanifanyia kitu mimi halafu
anaogopa Gardner atamnywesha sumu na hii ilikua maalum kwa ajili yake,
kwanza sisomagi magazeti ya aina hiyo ndio maana sikua naelewa hata
mnaongelea nini... Ieleweke hivyo, mimi sio MUNGU wala sina haki ya
kuhukumu bila uhakika
Comments 156, likes 221
Agosti 1
Captain G Habash anarudi Radio. Atasikika kuanzia September 1, 2012...Stay tuned, kujuaa jina la kipindi na Radio gani !!!
Comments 148, likes 280
Fid Q
Agosti 18
Eid Mubarak to ya all......... Love always!!!!
Comments 158, likes 433
Agosti 17
Leo
kwenye Fidstyle Friday tutapelekwa Mwanza kuona mauaji ya 'Young
Killah a k a Lil K' kuanzia saa tatu na nusu ya usiku huu ndani ya EATV
pekee..!! JOIN THE REVOLUTION
Comments 129, likes 221